Wednesday, 12 March 2014

HIDAYA




Mpendwa bibi alitueleza kuhusu ubinti
Hila yako mpyaro endelea, huniondoi ubichi
Mpujufu wewe hata uwezo wako sichafuki
Mwili wangu nimeukwatua sitaki utanguzi.

Kuanzia maisha yangu ndugu yangu sija…
Hata sasa sio mtoto tena bila haja
Si kila siku kunikumbusha mapenzi yako kwa kutaja
Ndugu yangu tulia, baadaye utashukuru hili tija.

Sio siri kwani miye manzi wa maana
Jamani nakusihi kwa sasa nipe yangu adhama
Ukristo umenifunza kuishi nah ii adhana
Sitojali yako chuki,kunayenipenda namanya.

Sikupi nafasi hata ng’o ya kunichafua
Kuhusu hayo mahaba kwa wote natanzua
Shamba langu linammoja ambaye atalikatua
Sitaki kukosa nguvu kwa sababu ya kunitanua.

Uhusiano wetu uishe tafadhali wacha kunifuata
Sitaki maisha yangu yaharibike au yaingie tata
Naona ni heri tusishirikiane katika kwata
Samahani,nakusikitisha kwani dhamira yako imedata.
   JIUZE GHALI DADA.

No comments:

Post a Comment